Marekani yatuma wanajeshi 400 nchini Syria

Marekani imewatuma wanajeshi  400 zaidi nchini  Syria ili kusaidia vikosi vya pamoja nchini humo vinavyolenga kutwaa tena ngome iliyotwaliwa na kundi la  Islamic State ya Raqqa. Wanajeshi hawa wanajumuisha vikosi vya wanamaji ambavyo viliwasili nchini humo siku chache zilizopita. Vikosi maalum vya Marekani tayari vimewasili nchini Syria. Wakati huo huo vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani vilitekeleza mashambulizi ya angani na kuwaua raia 20 wakiwemo watoto karibu na mji mmoja nchini humo.