Marekani yatishia kuwekea vikwazo wanaozuia uchaguzi mkuu Congo.

Marekani imetishia kumwekea vikwazo zaidi mtu yeyote ambaye anazuia uchaguzi kufanywa katika Jamhuri ya Congo, uchaguzi ambao tayari maandalizi yake yamecheleweshwa ili kuchukua mahala pa rais Joseph Kabila. A�Rais wa tume ya uchaguzi nchini A�humo anasema uchaguzi huo ambao ungelifanywa mwezi Novemba mwaka uliopita huenda usifanyike mwaka huu kutokana na kucheleweshwa kwa usajili wa mamilioni ya wapiga kura. Kucheleweshwa zaidi kwa uchaguzi huo huenda kukazua ghasia zaidi kufuatia maandamano dhidi ya serikali mwaka uliopita ambapo vikosi vya usalama viliwauwa mamia ya waandamanaji. Upinzani ulikatalia mbali tangazo la siku ya Jumapili ukisema A�linaweza kuzua machafuko zaidi katika Jamhuri ya Congo. Marekani mwaka uliopita iliwawekea vikwazo maafisa kadhaa wa serikali ya Congo na kuzuilia rasilimali zao za kifedha nchini Marekani na pia kuwazuia raia wa Marekani kutekeleza shughuli zozote za kifedha na watu hao.