Marekani Yashirikiana Na Wanariadha Wa Kenya Kukabiliana Na Ukimwi

Serikali ya Marekani imeshirikiana na wanariadha wa hapa nchini kwenye kampeni ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi hapa nchini. Akiongea katika hospitali kuu ya kaunti hukoA�A� Iten balozi wa marekani hapa nchiniA� Robert Godec amesema wanariadha wanawakilisha serikali ya Kenya katika kutoa uhamasisho kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi ili kukabiliana na ugonjwa huo.A� Godec alizuru hospitali hiyo na kuandaa mkutano na baadhi ya wanariadha wakiwemoA� Asbel Kiprop, Brimin Kipruto, Mercy Jerono, Edna Kiplagat, Ivy Kiyeng, Mary Keitany, Geofry Kamwaro, Emmanuel Mutai, naA� Stephen Kiprotich miongoni mwa wengine. Ushirikiano huo unalenga kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na kukabiliana kikamilifu na ugonjwa huo hapa nchini.A� Amesema wanariadha hao wako katika nafasi nzuri ya kuwafahamisha watu kubadili mitindo yao ya maisha. Aidha balozi huyo ametambua juhudi za serikali ya Kenya za kukabiliana na ugonjwa huo hapa nchini. AmempongezaA� hasa mama wa taifaA� Margaret Kenyatta kutokana na kampeni yake ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo kutoka kwa mama hadi kwa mtoto .A� Naibu gavana wa kaunti hiyoA� Gabriel Lagat ambaye alimkaribisha Godec amesema serikali ya Marekani haijashirikiana tu na serikali ya kaunti hiyo katika sekta ya afya bali pia katika sekta ya kilimo.