Marekani yashambulia Syria

Marekani imetekeleza mashambulizi ya makombora dhidi ya ngome kadhaa nchini Syria ili kujibu shambulizi linaloshukiwa kuwa la zana za kikemikali katika mji mmoja unaosemekana kudhibitiwa na waasi. Afisa A�wa makao makuu ya jeshi la Marekani ya Pentagon amesema kuwa makombora 50 yalirushwa katika eneo la mashariki mwa Mediterrenean katika ngome moja ya jeshi la angani la Syria. Haya yanawadia baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa hatua inafaa kuchukuliwa dhidi ya uongozi wa Syria. Mamia ya raia wanahofiwa kufariki katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la gesi ya sumu lililotekelezwa siku ya jumanne. Mapema siku ya alhamisi waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson amesema kuwa kiongozi wa Syria Bashar al-Assad hapaswi kutekeleza jukumu lolote A�katika uongozi wa baaadaye wa taifa hilo.