Marekani yalaumu Urusi kwa Udukuzi Wa Mitandao

Ikulu ya White HouseA�huko Marekani imedai Rais Vladmir Putin wa UrusiA�alihusika moja kwa moja katika udukuzi waA�mitandao ulioathiri matokeo ya uchaguzi wa Marekani. Mshauri wa rais Barack Obama, Ben Rhodes, amesema rais Putin anahodhi mbinu za utenda kazi wa serikali yake na kwamba kuna uwezekano mkubwa alijua kilichokuwa kikiendelea.

Katibu anayehusika na maswala ya vyombo vya habari katika ikulu yaA�White House Josh Earnest aliongeza kuwa ni bayana kwamba Putin alihusika katika njama hiyo licha ya maafisa wa serikali yake kukanusha vikali madai hayo. Urusi imepuuzilia mbaliA�A�uchakachuaji waA�A�habari na takwimu zilizoshawishi matokeo ya uchaguzi wa urais huko Marekani, huku chama cha Democratic kinapoendelea kujiuliza ni kwa nini mgombea urais wake Bi. Hillary Clinton alishindwa kwenye uchaguzi huo? Kwa sasa kidole cha lawama kimeelekezewa Urusi kulingana na mitazamo binafsi ya watu.