Marekani kupiga marufuku ubebaji vifaa vya kieletroniki safarini za ndege kutoka Afrika

Marekani imepiga marufuku ubebaji wa vifaa vya elektroniki kwenye ndege zinazosafiri kutoka mataifa manane ya mashariki ya kati na Afrika kaskazini,agizo ambalo lilitolewa kufuatia ripoti ya uchunguzi wa kijaasusi ngambo. Habari zilizotolewa na afisa mmoja wa serikali ya Marekani zinasema hatua hiyo itaathiri mashirika tisa ya ndege yanayoendesha shughuli zao katika viwanja kumi vya ndege nchini humo.Vifaa hivyo vilivyopigwa marufuku ni pamoja na vipakatalishi,kamera za Tablet,DVD na vifaa vya michezo ya elektroniki lakini sio simu za mkononi.Idara ya usalama wa ndani ilikataa kuzungumzia kuhusu suala hilo lakini inatarajjiwa kutoa tangazo leo. Mwezi uliopita ndege moja ya shirika la ndege la Daallo lenye makao yake huko Dubai iliharibiwa na mlipuko uliotokea punde tu baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji mkuu wa Somalia , Mogadishu.Wachunguzi wanasema abiria mmoja kwenye ndege hiyo alikuwa amebeba bomu la kipakatalishi.Rubani wa ndege hiyo alifanikiwa kutua na muathiriwa wa pekee alikuwa abiria huyo.Kundi la wapiganaji la al-Shabaab lilidai kuhusika na shambulizi hilo na uwezekano wa mashambulizi mengine kama hayo ndilo kero kwa maafisa wa kijaasusi wa Marekani.

A�