Marekani kuongeza zana za kinuklia.

Rais Donald Trump wa marekani amesema anataka nchi hiyo iongeze silaha zake za kinuklia kwenye kauli yake ya mwanzo kuhusu swala hilo tangu alipoanza wadhifa huo. Akiongea na shirika la Reuters kwenye mahojiano, Trump alisema ingekuwa bora iwapo hakuna nchi yoyote iliyo na silaha za kinuklia lakini akakariri haja ya marekani kusalia kuwa nchi iliyo na uwezo mkubwa wa kinuklia duniani. Alisema kuwa uwezo wa kinuklia wa nchi hiyo umepungua. Wakosoaji wanasema kuwa nchi za urusi na marekani zina silaha nyingi zaidi kuliko zinazohitajika kuzuia shambulizi la kinuklia.A� Shirika la kuthibiti umiliki wa silaha nchini marekani limesema kuwa nchi hiyo ina silaha 6,800 za kinuklia nayo urusi ina silaha elfu-7.