Marekani kuongeza idadi ya wanajeshi wake Afghanistan

Rais Donald Trump wa Marekani  amesema kuwa kuna uwezekano wa taifa hilo kuongeza idadi ya wanajeshi wake huko Afghanistan , kama mbinu mpya ya kudhibiti  wanamgambo wa kiislamu katika sehemu hiyo. Ikiwa hatua hio itatekelezwa, basi huo utakuwa mzozo mrefu  wa kivita katika historia ya  taifa hilo ugenini. Kwenye hotuba aliotoa katika kituo kimoja cha kijeshi karibu na jiji la Washinton, Trump  alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mbinu mpya ya  kuzuia Afghanistan kuwa ngome ya wanamgambo wa kiislamu ambao wanapania kuishambulia Marekani. Hotuba hiyo imetolewa baada ya sera za taifa hilo kufanyiwa mchakato, hasa kuhusu  kujihusisha kwa Marekani katika  ulindaji wa usalama  huko Afghanistan. Sera ya Marekani inalenga  kudhibiti vitendo vya wanamgambo wa Taliban  katika eneo hilo.