Marekani Kuipa Nigeria Ndege Za Kivita Kupambana Na Bokoharam

Serikali ya Marekani inatafuta idhini ya kuiuzia Nigeria ndege 12 za kivita za muundo wa A-29 Super TucanoA� kuisaidia kwenye vita dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram.Afisa mmoja wa serikali ya Marekani ambaye jina lake halikutajwa,amesema serikali ya nchi hiyo pia imetenga raslimali zaidi kwa mipango ya ujasusi dhidi ya wanamgambo hao na piaA� kutoa mafunzo kwa jeshi la wanahewa la Nigeria.Kuimarika kwa ushirikiano katika maswala ya kijeshi kati ya Marekani na Nigeria ni ufanisi mkubwa kwa rais Buhari ,aliyechukua hatamu za uongozi mwaka uliopita na kuahidi kupambana na wanamgambo hao,ambao alisema kwa muda mrefu wamekuwa kero kwa nchi hiyoA� yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.

A�