Maraga asema mahakama imejiandaa kutatua kesi za uchaguzi mkuu

Jaji mkuu David Maraga amesema idara ya mahakama iko tayari kukabiliana na mizozo yoyote ambayo huenda ikatokana na uchaguzi mkuu wa tarehe nane mwezi agosti.Akiongea alipozuru mahakama kuu ya Eldoret, alisema mahakama imefanya kazi nyingi katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao na majaji, mahakimu na idara zingine ziko tayari kushughulikia mizozo yoyote ambayo huenda ikatokea kabla na baada ya uchaguzi mkuu.Alisema wawaniaji wa wanachama wa mabunge ya kaunty ndio wanaotarajiwa kuwa na malalamishi mengi zaidi.

A�A�Jaji mkuu aliwahimiza wakenya kuombea uchaguzi wa amani na akatoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuangazia sera zao kwa njia ya kizalendo na kuepuka kutoa matamshi ya uchochezi.