Maraga Ahojiwa Na Kamati Ya Bunge

Jaji Mkuu mteule David Maraga amepuzilia mbali kesi tatu ziliwasilishwa dhidi yake kuhusiana na jinsi alivyoshughulikia kesi kadhaa alipokuwa Jaji huko Nakuru. Maraga alisema hayo alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu maswala ya sheria. Fredrick Onyancha, Tom Biegon na Emmanuel Korir wanadai kwamba uteuzi wa Maraga hautakuwa wa haki kwani alifanya uamuzi ambao haukuzingatia misingi ya sheria na ulisababisha mrundiko wa kesi katika vikao vyake. Pia jaji huyo aliulizwa na wanachama wa kamati hiyo kuhusu jinsi atakavyoshughulikia kesi za ufisadi katika idara ya mahakama. Ikiwa uteuzi wake utaidhinishwa na kamati hiyo ya bunge, Maraga atateuliwa rasmi na rais Uhuru Kenyatta kuwa jaji mkuu mpya.