Manusura wa Shambulizi la Kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa Watembelewa

Huku wakenya wakiadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea kwa shambulizi la kigaidi katika chuo kikuu cha Garissa, manusura wa mkasa huo kutoka kaunti ya Makueni walitembelewa na viongozi wao katika chuo kikuu cha Moi huko Eldoret.

Hayo yanawadia mwaka mmoja tangu magaidi kuvamia chuo kikuu chaA�A�Garissa na kuwaua watu wapatao 148 na kuwajeruhi wengine 79.

Mkewe gavana wa kaunti ya Makueni Nazi Kivutha alisema kuwa waliwatembelea wanafunzi 37 kutoka kaunti hiyo ili kuwaunga mkono na kuwahimiza tangu wajiunge na bewa kuu la chuo kikuu cha Moi. Wanafunzi hao walipewa ushauri nasaha na wataalamu ambao waliandamana na viongozi hao. Waliandaliwa dhifa na kukabidhiwa shilingi elfu 20 kila mmoja kama na serikali ya kaunti hiyo.