Manowari ya Marekani yawasili Korea Kusini

Manowari moja ya Marekani imewasili nchini Korea Kusini huku kukiwa na wasiwasi kuhusu tishio la Korea Kaskazini la kutekeleza shambulio la kinyuklia. Manoari hiyo kwa jina USS Michigan iliyo na makombora ya kinuklia itaungana na meli ya kivita ya Carl Vinson. Korea Kaskazini leo inaadhimisha miaka-85 ya kuanzishwa kwa jeshi lake. Katika siku zilizopita Korea Kaskazini imekuwa ikiadhimisha siku hiyo kwa kufanyia majaribio makombora ya kinuklia. Hofu imetanda katika eneo la Korea baada ya Marekani na Korea Kaskazini kujibizana vikali. Na katika hatua isiyo ya kawaida, wanachama wa bunge la Senate nchini Marekani kesho watahudhuria kikako cha kujadili Korea Kaskazini katika ikulu ya White House.