Manchester United yabaduliwa katika mashindano ya ligi ya vilabu bingwa barani ulaya

Timu ya Manchester UnitedA� inayoyoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza, ilibanduliwa katika kinyanga��anyiro cha ligi ya kilabu bingwa barani Ulaya jana usiku; baada ya kufungwa na Sevilla ya Uhispania, mabao mawili kwa moja.

Mchezaji wa ziada Wissam Ben Yedder ndiye aliyeifungia Sevilla mabao mawili yaliyoipa timu hiyo ushindi, dakika za 74 na 78, naye Romelu LukakuA� akaifungua United bao la kujiliwaza, dakika saba kabla ya mechi kukamilika. Manchester United imeondolewa katika kipute hicho sawa na Tottenham, lakini viongozi wa ligi ya Uingereza Manchester City, na Liverpool zilifuzu kwa mechi za robo fainali. Aidha, Chelsea itafuzu iwapo itaishindaA� BaselonaA� leo usiku.