Manchester United iko tayari kumsajili mshambulizi wa Brazil Carlos Vinicius kwa pauni milioni 35

Carlos Vinicius

Manchester United iko tayari kumsajili mshambulizi wa Brazil Carlos Vinicius kutoka kilabu cha Benfica kwa kima cha pauni milioni 35.

United inammezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyefunga mabao ishirini na matano kwenye michuano thelathini na mitatu msimu huu.

Nyota huyo ambaye anaongoza kwenye orodha ya wafungaji mabao mengi kwenye ligi kuu nchini Ureno pia ananuiwa kusajiliwa na viongozi wa ligi kuu Uingereza Liverpool.

Nyota huyo aliyejiunga na Benfica kwa kima cha pauni milioni 15 msimu jana alitia saini mkataba utakaokamilika mwaka 2024 kilabuni, ingawa amewekewa kitita cha pauni milioni 88 kwa kilabu kitakachotaka kumsajili.

Ripoti zinaarifu kuwa Man United ilikuwa inadai kuijaribu Benfica kwa kuilipa pauni milioni 35 ili kumsajili nyota huyo.