Manchester City kunuia ushindi wa 15 itakapochuana na Swansea City

Manchester City itanuia kupata ushindi wa kumi na tano mtawalia ligini itakapochuana na Swansea City uwanjani Liberty, huku ligi kuu nchini Uingereza ikirejelewa leo usiku.Kufuatia sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Everton siku ya Jumapili, Liverpool, inayoshikilia nafasi ya nne jedwalini, itacheza dhidi ya West Bromwich Albion uwanjani Anfield. Tottenham Hotspurs itakabiliana na Brighton huku Asenali ikimenyana na West Ham United. Manchester United itakuwa nyumbani dhidi ya Bournemouth, huku ikinuia kupunguza pengo kati yake na vinara Manchester City.