Mamia ya raia wa Togo watorokea nchini Ghana kukwepa kukamatwa

Mamia ya raia wa Togo wametorokea nchini Ghana kukwepa kukamatwa baada ya wimbi la maandamano dhidi ya serikali. Kundi la kwanza la raia hao liliwasilisha Ghana hapo jana na limepewa makazi katika wilaya ya Chereponi, karibu na mpaka kati ya Togo na Ghana. Afisa mkuu tawala wa wilaya ya Chereponi, Abdul Razak Tahiru aliwaambia wana-habari kuwa chakula, malazi na vyandarua vimegawiwa wakimbizi hao. Maelfu ya raia wa Togo wamekuwa wakifanya maandamano barabarani kushinikiza kujiuzulu kwa rais Faure Gnassingbe, ambaye alichukua hatamu za uongozi mwaka-2005. Maafisa wa usalama nchini humo walikabiliana na waandamanaji hao katika eneo la Mango ambapo mtu mmoja aliuawa na zaidi ya wengine-20 kujeruhiwa.