Joyce Kahiga

Dada Joyce Kahiga maarufu ‘Askofu’ si mgeni kwako wamtambua. Huendesha kipindi cha Mwamba wa Baraka kila Jumapili  kuanzia saa Kumi na moja hadi  nne mchana.Pia utampata kwenye Top Mashariki na Mwinyi Kazungu Mtetezi kila siku ya Juma.Ana sauti ya kumtoa nyoka pangoni. Aliwahi kukuletea kipindi cha PAMBO LA REDIO TAIFA ,ambacho pia alishirikiana na Mathias Momanyi  hivi sasa chaitwa VUVUZELA.

Tayari ana shahadi ya Diploma,na kwa sasa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Moi. Utapata uhondo!