Mambo Mbotela

Mambo Mbotela ni mtangazaji wa muda mrefu kwenya idhaa ya Kiswahili.Yeye ni mtayarishaji wa kipindi maarufu cha JE, HUU NI UUNGWANA?A�kwenye Redio na Televisheni. Alivutiwa na kazi ya utangazaji tangu akiwa shuleni.Kwa ajili ya ari yake katika fani hii,kwanza alianza kufanya kazi na gazeti la kiingereza la ‘Kenya Weekly News’ na hatimaye gazeti la Baraza la ‘East African Standard .’ Alijiunga na Shirika la KBC 1964. Amekuwa maarufu katika usomaji wa habari, matangazo ya kandanda na pia utangazaji wa zamu. Amewahi kufanya kazi na kitengo cha afisi ya habari za Rais A�yaani PPS. Kutokana na kazi hii amezuru sehemu nyingi za nchiA� na nchi za ng`ambo.Mambo anakumbukwa sana kwa wajibu aliotekeleza 1982 alipochukuliwa na wanamapinduzi wakitaka kupindua serikali ya rais mtaafu Moi.