Mama wa taifa azindua mpango ambao utaimarisha sekta ya kiafya

Mama wa taifa Margaret Kenyatta leo atazindua mpango ambao utaongoza juhudi zake za kuimarisha sekta ya afya katika muda wa miaka mitano ijayo.Mpango huo utazingatia  zile ajenda  nne kuu zinalolenga kutoa  huduma bora za afya kwa wakenya wote,uzalishaji wa chakula cha kutosha,ujenzi wa nyumba za bei nafuu pamoja na kubuni nafasi zaidi za kazi. Mpango huo pia unalenga kudumisha ushirikiano na kutetea utaoji wa huduma bora za afya.Akiongea katika chuo kikuu cha Strathmore wakati wa mjadala wa kumbu kumbu wa  Adebisi Babatunde Thomas,mama wa taifa alisema juhudi za mpango wake wa Beyond Zero ziliokoa maisha ya wanawake wangi wajawazito pamoja na kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi ingawaje takwimu zinaonyesha kuwa mengi zaidi yanahitaji kufanywa.