Mama Wa Taifa Atarajiwa Kukabidhi Gari La 42 Lenye Kliniki Katika Kaunti Ya Busia

Mama wa taifa Margaret Kenyatta anatarajiwa kukabidhi gari la 42 lenye kliniki kwa kaunti ya Busia chini ya mpango wake wa Beyond Zero.Huduma za kina mama kujifungua bila malipo zimechangia ongezeko la idadi ya kina mama wanaojifungulia hospitalini katika kaunty ya Busia katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.Kulingana na afisa mkuu wa matibabuA� katika hospitali kuu ya kaunty ya Busia , Dr. Janerose Ambuchi, hospitali hiyo kufikia sasa imeshuhudia ongezeko la idadi hiyo kutoka kina mama 2,844 hadi 3,735 tangu kuzinduliwa kwa huduma ya kina mama kujifungua bila malipo mwaka 2013.Alisema,wakati wa kipindi hicho,idadi ya watoto waliozaliwa wakiwa hai iliongezeka kutoka 2742 hadi 3594 na idadi ya vifo kupungua kutoka 438 mwaka 2013 hadi 278 mwaka uliopita. Mkewe Rais ambaye yuko katika eneo la magharibi mwa Kenya leo atatoa kliniki ya 42 ya kuhudumu kwa gari ya mpango wa Beyond Zero kwa kaunty ya Busia. Dr. Ambuchi alisema kliniki hiyo itachangia huduma za afya zinazotolewa na kaunty ya Busia kwani itawafikia watu wanaoishi katika sehemu za ndani.Alikariri kwamba asilimia 40 ya wanawake wajawazito wanaotafuta huduma katika kaunty hiyo wanatoka nchi jirani ya Uganda.