Mali ya thamani yateketea baada ya mkasa wa moto kutokea huko Langata

Mali ya thamani isiojulikana iliteketea usiku wa kuamkia leo wakati moto mkubwa ulipoteketeza vijiji vilivyo karibu na A�mta wa Langata hapa Nairobi.Watu kadhaa wameachwa bila makao,huku manusura kadhaa wamehifadhiwa katika shule ya msingi ya Ngei.Akizungumza na KBC kwa njia ya simu leo alfajiri,mkuu wa polisi katika kaunti ya Nairobi Japheth Koome alisema kuwa hakuna mtu aliangamia kwenye mkasa huo wa moto,japo wengine walijeruhiwa walipokuwa wakijaribu kuokoa mali yao.Koome alisema polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo.Alisema huenda moto huo ulianzia kwenye mabanda ya eneo la Kijiji mkabala na mtaa wa Southlands na kuenea kwa haraka hadi sehemu zilizo jirani.Magari ya kuzima moto yalionekana yakijaribu kuuzima moto huo ,japo yalikosa njia za kupitia ili kuzifikia sehemu zilizokumbwa na janga hilo. Wazima moto walikuwa na wakati mgumu kufikia kitovu cha moto huo.