Mali Ya Thamani Kubwa Yaharibiwa Na Mafuriko Kisumu

Idara ya utabiri wa hali ya anga imewataka wakenya wajiandae kwa majira ya mvua ya masika katika miezi ya Machi, Aprili na Mei. Haya yanajiri huku mjiA�wa Kisumu ukishuhudia mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha mjiniA�humo na kuharibu mali ya thamani kubwa, mbali naA�kusababisha kupotea kwa stima.A�Mvua hiyo ilisababisha kufurika kwaA�barabara nyingi mjini humo.A� Jiji la Nairobi pia lilikumbwa na mvua Jumatano jioni. Idara hiyo ya utabiri wa hali ya anga imesema kwamba mvua hiyo ya masika inatarajiwa kuanza katika juma la pili au la tatu la mwezi huu katika maeneo mengi ya magharibi mwa nchi huku sehemu nyingi za mashariki mwa nchi hasa kaskazini mashariki huenda yakapokea mvua hiyo katika A�juma la kwanza hadi la pili la mwezi Aprili. Hata hivyo, sehemu nyingi nchini zinatarajiwa kupokea kiasi kidogo cha mvua hasa kwenye eneo la mashariki mwa nchi katika kipindi hicho