Moto waharibu mali ya mamilioni ya pesa Kinoo

Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa iliharibiwa jana usiku na moto uliozuka katika eneo la kibiashara la Kinoo katika kaunti ya Kiambu. Moto huo uliteketeza kabisa vibanda vya wafanyibiashara wa eneo hilo. Imebainika kuwa moto huo ulianza wakati kibanda kilichokuwa kikigawanywa na mchoma vyuma kiliposhika moto kabla ya moto huo kusambaa hadi katika vibanda vingine. Mwakilishi wa wodi katika eneo hilo Samuel Kimani ambaye alizuru mahala pa mkasa huo, aliwahakikishia wafanyibiashara hao kuwa serikali ya kaunti ya Kiambu itatoa pesa zaidi za kununua magari ya kuzima moto kwa kila wodi ili kukabiliana na visa vya moto katika kaunti hiyo.A�Aliongeza kuwa hazina ya serikali ya kaunti ya kushughulikia maswala ya dharura itatumika kuwafidia walioathirika.