Malaysia kufutilia mbali mfumo wa raia wa Korea kuingia nchini humo

Malaysia itafutilia mbali mfumo wa raia wa Korea kaskazini kuingia nchini humo bila visa kuanzia tarehe 6 mwezi huu kwa mujibu wa shirika moja la habari nchini humo. Hii inafuatia kuzorota kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili kufuatia mauaji ya Kim Jong Nam katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.A� Naibu waziri mkuu Ahmad Zahid Hamidi alinukuliwa akisema kuwa raia wa korea kaskazini watalazimika kuwa na visa kabla ya kuingia nchini Malaysia kwa sababu za kiusalama.