Malalamiko Ndani Ya ODM Yasababisha Chama Hicho Kuratibu Mikakati Ya Kukabiliana Na Mizozo Ya Ndani

Chama cha (ODM) kimeratibu mikakati ya kukabiliana na mizozo ya ndani. Hii ni kufuatia malalamiko ya wabunge wawili kutoka eneo la magharibi mwa Kenya na pia maafisa wa chama hicho waliodai wamekuwa wakipuuzwa kuhusiana na usimamizi wa chama hicho. Katibu mkuu wa (ODM) Ababu Namwamba na makamu mwenyekiti wa chama hicho Paul Otuoma, wote kutoka Kaunti ya Busia, wameshtumiwa kwa kukihujumu chama hicho huku wakiegemea upande wa Jubilee. Hata hivyo mkutano uliofanyika jana chini ya uongozi wa kinara wa chama hicho, Raila Odinga na kuhudhuriwa na viongozi hao wawili haukujadili mzozo unaotishia kusambaratisha chama hicho. Akihutubia wana-habari baada ya mkutano huo, Namwamba alisema maswala yanayotishia umoja katika chama hicho yatashughulikiwa katika muda wa majuma mawili. Alisema mkutano huo wa kamati kuu ulijadili swala la marekebisho kwa tume ya (IEBC), na ukaazimia kuwaunga mkono wale watakaoteuliwa na kujaza nafasi ya Prof. Hellen Sambili ambaye amekataa kujiunga na kundi hilo.

Namwamba hakusema lolote kuhusu hatma yake katika chama cha (ODM). Ameripotiwa kupuuza mikutano na pia shughuli za (ODM) hivyo kuchangia uvumi kwamba anapanga kunga´┐Ż´┐Żatuka.