Makumi wapoteza maisha Nigeria kutokana na homa ya Lassa

Nigeria inakabiliwa na changamoto mbili za kiafya kufwatia kuzuka kwa A�homa ya Lassa,ambayo inafanana na ile ya Ebola ambayo imesababisha vifo vya watu 110 mwaka huu.Huku madaktari wakijishughulisha kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo,wataalamu wa afya wameshangazwa na kuenea haraka kwa ugonjwa huo katika kipindi kifupi.KItuo cha kitaifa cha kudhibiti magonjwa-NCDC kimethibitisha kuwa zaidi ya visa 353 vya ugonjwa huo vimetokea tangu tarehe mosi ,mwezi januari mwaka huu ikilinganishwa na A�visa 143 kwa mwaka mzima wa 2017.Hata hivyo imesemekana A�huenda sababu ikawa A�jinsi homa hiyo hatari inavyoenezwa kupitia kwa mkojo au kinyesi cha mgonjwa au panya ambaye amegusa kinyesicha muathiriwa.Japo inafanana na ile ya Ebola,homa ya Lassa haiambukizi kwa haraka.Hata hivyo wahudumu wa afya hawana budi kujikinga kikamilifu wanapowahudumia wagonjwa.