Makasisi Wakishifiwa Kwa Kusababisha Vifo Vatican

Mweka hazina katika mji wa Vatican kadinali George Pell ameahidi kusaidia kupunguza visa vya kujitia kitanzi miongoni mwa watu ambao wanasemekana kunyanyaswa na baadhi ya makasisi wa kanisa katoliki walipokuwa watoto. Kadinali Pell alikutana faraghani na kundi la manusura waliotorokea mjini Rome ili kushuhudia akitoa ushahidi katika tume moja ya Australia kuhusiana na dhulma dhidi ya watoto. Kadinali huyo alitoa ushahidi kutoka mjini Rome kupitia kwa mtandao wa video kutokana na hali yake mbaya ya kiafya. Msemaji wa manusura hao Gerard Ridsdale alisema kuwa walikuwa na mazungumzo ya kufana katika mkutano wa jana. Kundi hilo awali lilikuwa limekataa kukutana na Pell na lakini likakubali kukutana naye baada ya kuondolewa kwa masharti Fulani kuhusiana na mazungumzo hayo.