Makamu wa rais wa zamani wa Zibambwe Joice Mujuru ashambuliwa

 

Aliyekuwa makamu wa rais wa  Zimbabwe Joice Mujuru ameshambuliwa alipokuwa katika mkutano wa kisiasa  kwa mujibu wa chama chake.  Chama cha upinzani cha  National People’s kimesema kuwa  Mujuru na wengine kadhaa walishambuliwa kwa mawe akifanya kampeini katika mji mkuu wa taifa hilo  Harare.  Watu wanane walijeruhiwa na lakini majeraha ya Mujuru hayakuwa mabaya. Chama chake kinadai kuwa shambulizi hilo lilichochewa kisiasa.Mujuru alikuwa akipigiwa upato wakati mmoja kumrithi Robert Mugabe kabla ya kuondolewa kwa wadhifa wa makamu wa rais mwaka wa 2014. Inadaiwa kuwa hatua hiyo ilichochewa na mkewe Mugabe, Grace. Mujuru alifurushwa kutoka chama cha Zanu-PF na akatwaa urais wa chama cha National People’s.