Makaazi Wa Kisii Wahakikishiwa Usalama Wa Chanjo Inayoendelea Dhidi Ya Ugonjwa Wa Ukambi Na Rubella

Serikali ya kaunti ya Kisii imewahakikishia wakazi kuhusu usalama wa chanjo inayoendelea kutolewa dhidi ya ugonjwa wa ukambi na rubella.A� Akiongea leo katika shule ya msingi ya A�Kisii alipokuwa katika ziara ya kutathmini shughuli ya utoaji chanjo hiyo , mwanachama wa kamati kuu inayosimamia huduma za afya katika kaunti hiyo Sarah Nyamache amepuzilia mbali madai kuwa serikali inatumia chanjo hiyo kama chombo cha upangaji uzazi. Amesema chanjo hiyo imejaribiwa na kuthibitishwa na shirika la afya ulimwenguni kuwa salama kwa watoto.A� Nyamache ametoa wito kwa wananchi kuchukulia chanjo hiyo kwa uzito unaostahili akisema nchi hii ingali inakumbwa mara kwa mara na chamuko ya ugonjwa wa ukambi na Rubella.A� Amesema ni kinyume cha sheria kwa wazazi kuwanyima watoto wao haki ya kuchanjwa na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wazazi wanaofanya hivyo. Ameelezea matumaini kuwa kufikia mwishoni mwa shughuli hiyo kesho , kaunti hiyo itakuwa imeafikia lengo lake la kuchanja watotoA� 651,000 wa kati ya umri wa miakaA� 9 na 14.