Majimbo kadhaa Marekani yataendelea kupinga sheria za rais Trump

Majimbo kadhaa nchini Marekani yamesema kuwa yataendelea na harakati za kisheria dhidi ya sheria zilizofanyiwa marakebisho za rais Donald Trump ambazo zinawaekea maarufuku ya kuingia Marekani raia na wakimbizi kutoka mataifa sita ya kiislamu. Jimbo la Washington ambalo lilikuwa la kwanza kwenda mahakamani, lilidai kuwa sheria hizo mpya zinakiuka katiba na kuwabagua waislamu. Mwanasheria mkuu wa jimbo hilo Bob Ferguson amesema kuwa hoja iliyotolewa na afisi yake inataka amri hiyo kufutiliwa mbali.

A�