Majaji Wapya Waapishwa

 

Majaji wapya 28 wameapishwa.19 kati yao watahudumu katika kitengo cha mazingira na ardhi.Hafla ya kuapishwa kwao ilishuhudiwa na rais Uhuru Kenyatta aliyetumai kuwa kesi za ufisadi nchini sasa zitasikizwa na kuamuliwa kwa wakati ufaao kufuatia kuapishwa kwa majaji wapya. Rais alisema kuapishwa kwa majaji hao kutasaidia pakubwa kwenye vita dhidi ya ufisadi.Pia alitumai kuwa kesi kuhusu ardhi zilizoko mahakamani pia zitashughulikiwa upesi kwa vile zimekuwa kizingiti kwa juhudi za serikali za kuwavutia wawekezaji zaidi.Alimhakikishia jaji mkuu David Maraga kuwa serikali itaunga mkono idara za mahakama katika majukumu yake ya kuwatendea haki wakenya .Waliopishwa ni Onyiego John Nyabuto, Cherere Thrispisa, Wanjiku Wamae, Ogola Daniel Ogembo, Gitari Lucy Waruguru, Ngetich Rachel Biomondo, Kemei David Kipyegomen, Onginjo Anne Colleta Apondi, Matheka Teresia Mumbua na Nyagah Jesse Njagi miongoni mwa wengine.