Majaji wa mahakama ya rufani wanakutana mjini Mombasa

Majaji wa mahakama ya rufani wanakutana mjini Mombasa kushauriana kuhusu maono ya mahakama hiyo ili kuimarisha utoaji huduma. Mkutano huo wa siku tatu wenye maudhui: a�?maono ya mahakamaa�� utajidili utumiaji mfumo wa dijitali katika mahakama hiyo, maadili ya idara ya mahakama, usimamizi wa mahakama na upatanishi na pia taaluma ya sheria za kibinadamu zinazoibuka na zile zinazokinzana katika maswala yanayohusiana na leba. Majaji hao kutoka kaunti za Nairobi, Malindi, Nyeri na KisumuA� pia wataangazia taratibu za usuluhishaji wa mizozo ya kiuchaguzi na mikakati ya kukomesha mrundiko wa kesi katika mahakama hiyo miongoni mwa maswala mengine. Akiongea kwenye mkutano huo rais mpya wa mahakama ya rufani, Jaji William Ouko alitambua uimarishaji shughuli za mahakama na A�kuimarisha ushirikishi wa wadau kuwa baadhi ya maswala muhimu ambayo mahakama hiyo itayaangazia ili kuimarisha ubora. A�Alisema hii ni muhimu katika kuafikia maono ya mahakama hiyo ya kuwa na mahakama yenye usawa, inayoamua k kesi kwa haraka, ya kitaalamu na yenye utenda kazi bora.