Maisha Ya Abiria Zaidi Ya Sitini Wa Ndege Kuhatarishwa

Somalia imezindua uchunguzi baada ya ndege moja kutua kwa dharura katika mji mkuu wa taifa hilo Mogadishu ikiwa na shimo kubwa katika kiunzi chake.A� Kulikuwa na hofu kuwa huenda shimo lililokuwa katika ndege hiyo iliyokuwa ikielekeaA� Djibouti lilisababishwa na bomu. Ripoti zaarifu kuwa mtu mmoja alianguka kutoka kwa shimo hilo ambalo lilionekana baada ya ndege hiyo kuondoka katika uwanja wa ndege wa Mogadishu. Shirika la ndege la Daalo limesema kuwa abiria wote sitini waliokuwa katika ndege hiyo wako salama isipokuwa abiria wawili walijeruhiwa katika kisa hicho