Maina Kiai Kutuzwa na Umoja Wa Mataifa

Mwakilishi maalum wa umoja wa mataifa kuhusu haki na uhuru wa kukongamana na kushirikiana kwaA� amani Maina Kiai atapokea tuzo la haki za binadamu la umoja wa mataifa la wakfu wa Leo NevasA� tarehe 18 mwezi huu.A� Kiai atapokea tuzo hilo katika dhifa ya chakula cha jioni ya wakfu wa Global Leadership mjini New York juma lijalo. Tuzo hilo linaenzi kazi ya Kiai ya kutetea haki za kiraia akiwa mwakilishi maalum wa umoja wa mataifa. Amehudumu kwenye wadhifa huo tangu tarehe mosi mwezi Mei mwaka wa 2011. Kiai alisema kwenye taarifa kwamba amenyenyekezwa kupokea tuzo la mwaka huu la Leo Nevas kwa kazi yake. Wengine watakaotuzwa kwenye hafla hiyo ni pamoja na rais Barrack Obama wa Marekani ambaye atapokea tuzo la wakfu huo la kuongoza harakati za kuleta mabadiliko duniani na Ertharin Cousin, mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula duniani-WFP. Tuzo la Leo Nevas la haki za binadamu lilizinduliwa na jopo la kutetea haki za binadamu la Leo Nevas mwaka wa 2007 kwa heshima ya mwanachama wa bodi hiyo aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi Leo Nevas, ambaye ni wakili wa kutetea haki za binadamu. Umaarufu ya Kiai kwenye kazi ya kutetea haki za binadamu ulianza alipokuwa mkurugenzi mkuu muasisi wa tume ya haki za binadamu hapa nchini mwaka wa 1992.