Mahakma Yasimamisha Tume Ya IEBC Kuendeleza Mipango Ya Kuchapisha Makaratasi Ya Kura

Tume huru ya uchaguzi na mipaka imezuiwa kuandaa uchaguzi wa chama cha wanasheria hapa nchini uliopangiwa kufanyika tarehe-25 mwezi huu. Hii ni baada ya mmoja wa wawaniaji nyadhifa kwenye uchaguzi huo kuelekea mahakamani akidai kuwa amenyimwa fulsa ya kushiriki kwenye uchagzui huo. Jaji Weldon Korir wa mahakama kuu ya Milimani alisema rufaa yaA�Frank Ochieng Walikwe anayetaka kuwania wadhifa wa mwanachama wa baraza la kitaifa cha chama cha LSK inapaswa kusikilizwa na kuamuliwa kabla ya uchaguzi huo kuandaliwa. Aliagiza tume ya IEBC isichapishe karatasi za uchaguzi hadi rufaa hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa. Aidha, mlalamishi huyo aliagizwa kuwasilisha karatasi za rufaa hiyo kwa chama cha LSk na tume ya IEBC huku swala hilo likitarajiwa kusikilizwa baina ya pande husika mnamo jumatano.