Magavana watakiwa kutia saini mkataba na madaktari

Mahakama ya rufaa imeagiza baraza la magavana na wizara ya afya kutia saini mkataba wa utambuzi , makubaliano ya pamoja na makubliano ya kurejea kazini na madaktari kufikia Jumatatu wiki ijayo. Kundi la wapatanishi linaloongozwa na viongozi wa kidini limepatiwa siku tatu zaidi kushughulikia maswala machache yaliyosalia na kuafikia makubaliano ya kurejea kazini na madaktari. Mahakama ya rufaa imewahimiza viongozi wa kidini kushirikiana na viongozi hadi suluhu ipatikane. Wakili A�Philip Murgor anayewakilisha maafisa wa chama cha wahudumu wa matibabu na wataalam wa meno hapa nchini (KMPDU) A�amesema kinachosalia sasa ni kwa pande husika kuafikiana kuhusu jinsi ya kushughulikia mkataba wa pamoja wa mwaka 2013 unaokumbwa na utata na kuafikia makubaliano ya kurejea kazini na kuongeza kuwa makubaliano hayo yanajadiliwa. A�Amesema makubaliano ya utambuzi yanafaa kutiwa saini kwanza kabla ya kuafikiwa kwa makubaliano ya kurejea kazini na kisha kushughulikiwa kwa mkataba wa pamoja wa mwaka 2013. A�Hata hivyo baraza la magavana limesisitiza kuwa madaktari wanafaa kurejea kazini kwanza kabla ya kutiwa saini kwa mkataba wa utambuzi katika muda wa siku tano na kufuatiwa na mkataba huo wa pamoja katika muda wa siku kumi.