Mahakama Yapata Faili Ya Dedan Kimathi Kutoka Uingereza

Nakala iliyoidhinishwa ya kesi iliyofanyiwa Dedan Kimathi na faili ya rufani kutoka Uingereza sasa zimo hapa nchini. Faili hiyo ambayo ilikuwa imehifadhiwa katika idara ya mahakama ilipatikanaA� kutoka maktaba ya bunge la Senate ya chuo kikuu cha London wiki iliyopita. Faili hiyo inahusu kesi ya mwaka 1956 na hukumu iliyotolewa kwa marehemu mpiganiaji ukombozi huyo huko Nyeri ambako alikuwa ameshtakiwa kwa kupatikana na bunduki kinyume cha sheria na hatimaye akahukumiwa kifo na kifungo gerezani na kazi ngumu kwa hatia hiyo. Faili hiyo ya Kimathi itakuwa miongozi mwa vifaa nadra katika makavazi mpya ya idara ya mahakama hapa nchini ambayo itafunguliwa hivi karibuni katika jengo la mahakama ya juu. Makavazi hiyo itakuwa na habari na vifaa vinavyoangazia matukio ya kihistoria katika idara ya mahakama hapa nchini.