Mahakama Yakataa Ombi La Mbunge Wa Gatundu Kusini Kuzuia CORD Kuandaa Maandamano

Mahakama kuu imekataa kuidhinisha ombi la mbunge waA�A�Gatundu Kusini, Moses Kuria la kuzuia upinzani kuandaa maandamano dhidi ya tume ya IEBC. Jaji Joseph Onguto alisema maandamano ya amani ni haki iliyoratibishwa kwenye katiba. Aidha mahakama hiyo iliagiza polisi kuwapa ulinzi wanaoshiriki katika maandamano dhidi ya tume ya IEBC. Katika ombi lake, Moses Kuria aliitaka mahakama izuie upinzani kuvamia afisi za tume hiyo ya uchaguzi na mipaka kuwatimua makamishna wake kwani hatua hiyo ni kinyume cha katiba.A�A�Uamuzi huo umejiri saa chache tu kabla ya viongozi wa CORD kuanza maandamano yao ya kushinikiza kuondolewa afisini kwa makamishna wa IEBC.