Mahakama Yaagiza Waziri Wa Fedha Kusimamisha Usambazaji Wa Shilingi Bilioni 25

Mahakama kuu imeiagiza waziri wa fedha kusimamisha usambazaji shilingi bilioni-25 kwa hazina ya ustawi wa maeneo bunge.Jaji wa mahakama kuu Joseph Onguto amemwagiza waziri wa fedha A�Henry Rotich kutotoa pesa hizo hadi kesi iliyowasilishwa mahakamani na wanaharakati wawili wa haki za binadamu A�Wanjiru Gikonyo na Cornelius Oduor kupinga uhalali wa hazina hiyo itakaposikizwa na kuamuliwa.Wakati huo huo mbunge wa Eldama Ravine ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya hazina hiyo kwenye bunge la taifa kutafakari manufaa yaliopatikana hapa nchini kutokana na pesa hazina hiyo,hasa sehemu za mashambani.