Mahakama ya juu yaonya umma kuhusiana na rufaa ya matokeo ya urais

Idara ya mahakama imeonya pande zote husika kwenye kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais, kujiepusha na kuzungumuzia kesi hiyo nje ya mahakama. Mahakama ya juu pia ilionya umma dhidi ya kutoa matamshi ambayo huenda yakaonekana ni kama yanaelekeza mahakama hiyo jinsi ya kuendesha kesi hiyo. Kwenye taarifa, mahakama ya juu pia imevitaka vyombo vya habari pamojaA� wanahabari binafsi kuhakikisha kuwa hawapendelei upande wowote wakati wanaporiti kuhusu rufaa hiyo.Taarifa hiyo ilikariri kwamba wanahabari lazima wazingatie maadili ya taaluma yao wakati wowote.Mahakama hiyo iliongeza kwamba matamshi ambayo yanamlenga jaji wowote kwa njia isiyofaa hayatavumiliwa.Mahakama hiyo imewataka mawakili wote kuwashauri wateja wao kuhusu swala hilo ikiwemo hatua zitakazochukuliwa dhidi yao endapo watakiuka masharti hayo.Mahakama ya juu ilikariri kwamba inasimama kidete na wakenya katika kutambua umuhimu wa kufikia kauli muafaka kuhusiana na rufaa hiyo.