Mahakama ya juu nchini Marekani kuidhinisha vikwazo vya usafiri vilivopendekezwa na Trump

Mahakama ya juu nchini Marekani imeidhinisha kutekelezwa kikamilifu kwa vikwazo vya usafiri viliyopendekezwa na rais Donald Trump dhidi  ya  mataifa sita ya kiislamu ambayo ni Chad ,Iran,Libya, Somalia ,Syria na Yemen.Hata hivyo agizo hilo lingali linakabiliwa na changamoto kadhaa za kisheria.Uamuzi huo ni sehemu ya agizo lililotolewa na rais Trump aliposhika hatamu za ungozi wa Marekani.Siku ya jumatatu,jopo la majaji 9 lilifutilia mbali sehemu ya  sheria hizo iliopitishwa na mahakama ya chini.Mahakama za rufani  huko San Francisco,Carlifonia , Richmond na Viginia yatasikiliza kesi kuhusu sera hizo na kubaini ikiwa  zina mashiko kisheria.