Mahakama kuu yafutilia mbali zabuni ya shilingi bilioni 2.5 ya IEBC

Mahakama kuu imefutilia mbali zabuni ya tume ya IEBC ya shilingi bilioni-2.5 iliyotolewa kwa kampuni yaA�Al Ghurair huko Dubai kuchapisha karatasi za kupigia kura. Akifutilia mbali zabuni hiyo, jajiA�George Odunga alisema kampuni hiyo haikuafiki kanuni za sheria mpya ya uchaguzi ya mwaka-2016. Jaji Odunga hivyo basi ameiagiza tume hiyo inayoongozwa na Wafula Chebukati kuanzisha upya utaratibu wa kutoa zabuni hiyo kulingana na sheria ya usambazaji na uwasilishaji karatasi za uchaguzi, matokeo ya uchaguzi, fomu na sajili. Wakili wa A�CORD James Orengo alipinga kandarasi hiyo akisema maelezo kuhusu vifaa hivyo vya uchaguzi kwenye hati za zabuni hayakuambatana na sheria ya uchaguzi iliyorekebishwa na mfumo wa kielektroniki uliotangamanishwa.Tume ya uchaguzi ilipinga kufutiliwa mbali kwa zabuni hiyo ukisema utacheleshwa maandalizi ya uchaguzi.