Mahakama kuu imeagiza kuondolewa kwa jina la Rais kwenye kesi

Mahakama kuu imeagiza kuondolewa mara moja kwa jina la Rais kwenye kesi iliyowasilishwa na mwanaharakati Okiya Omtatah kuhusu kubuniwa kwa wadhifa wa makatibu wasimamizi wa wizara. Justice Chacha Mwita alipitisha uamuzi kwamba Rais hawezi kushtakiwa kwani katiba imempa kinga ya kushtakiwa. Mwanaharakati huyo alikuwa amemshtaki Rais na tume ya kuwaajiri watumishi wa umaA�A�kwa kukiuka katiba alipoanzisha wadhifa huo bila kuhusisha uma.Hatahivyo mkuu wa sheria alifanikiwa kuwasilisha ombi la kutaka jina la Rais liondolewe kwenye kesi hiyo huku akiwaacha washtakiwa wengine wajitetee.