Aliyekuwa Rais Wa Chad Asubiri Maamuzi Kuhusu Rufaa Ya Kifungo Chake

Mahakama maalum ya muungano wa Afrika imesema jana kuwa itatoa uamuzi wake kuhusu rufaa iliyotolewa kwa niaba ya aliyekuwa rais wa Chad Hissene Habre kupinga kifungo cha maisha dhidi yake tarehe 27 mwezi Aprili mwaka huu. Kikao maalum kilichobuniwa na Senegal na muungano wa Afrika, kilimhukumu A�Habre mwezi Mei kifungo cha maisha kwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu. A�Mawakili walioteuliwa kumwakilisha A�Habre na mahakama hiyo walikataa rufaa kwa niaba yake siku ya jumatatu licha ya kuwa kiongozi huyo wa zamani wa kihimla mwenye umri wa miaka 74 amekataa kutambua mamlaka ya mahakama. A�Hata hivyo vikao vya mahakama vimeendelea bila kuwepo kwa Habre na mahakama itatoa uamuzi wake tarehe 27 mwezi Aprili kwa mujibu wa rais wa mahakama ya rufaa A�Wafi Ougadeye. Iwapo uamuzi huo wa mahakama utadumishwa, A�Habre atahudumia kifungo chake nchini Senegal au katika taifa lingine la muungano wa Afrika.