Mahakama Kuidhinisha Matumizi Ya Hazina Ya CDF Eneo Bunge La Ganze

Bodi inayosimamia hazina ya CDF katika eneo bunge la Ganze imepewa idhini na mahakama kutumia pesa zilizotengewa miradi mbali mbali ya maendeleo katika eneo hilo .Mahakama ilikuwa imesimamisha matumizi ya pesa za hazina hiyo mwezi Novemba mwaka 2014 kufuatia ubishi kati ya baadhi ya wanachama wa bunge la kaunti ,na mbunge wa eneo hilo Peter Shehe kuhusiana na matumizi ya pesa hizo .Akiongea kwenye mkutano wa kamati ya kushirikisha mipango ya kuboresha huduma huko Ganze,naibu wa kamishna wa kaunti ya Kilifi Wilson Ole Saaya alisema miradiA� kadhaa ,hasa ya ujenzi wa shule iliyokuwa imesimamishwa kufuatia agizo hilo la mahakama sasa itaendelea .Hata hivyo aliwahimiza viongozi wa sehemu hiyo kuweka kando tofauti zao za binafsi na kushirikiana kwa minajili ya maendeleo ili kuinua hali ya maisha ya wakazi.Kadhalika aliwataka wanachama wa bodi hiyo ya CDF kuendesha shughuli zake kwa uadilifu