Mahakama kuamua kuhusu hatua ya Uingereza kuiuzia Saudi Arabia Silaha.

Mahakama moja kuu inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa biashara ya uingereza ya kuiuzia silaha Saudi Arabia. Mahakama hiyo itaamua iwapo serikali ya uingereza ilikosa kusitisha uuzaji wa silaha kwa ufalme wa Saudi Arabia ambayo inakabiliana na vita nchini Yemen. Umoja wa mataifa umedai kwamba mashambulizi ya angani ya Saudi Arabia dhidi ya waasi wa kundi la Houthi nchini Yemen yamesababisha vifo vya maelfu ya raia. Kundi moja linalotekeleza kampeni dhidi ya biashara hiyo ya silaha ambalo limewasilisha kesi hiyo limedai kwamba uingereza imekiuka sheria ya kibinadamu. Vifaa vilivyouziwa Saudi Arabia ni pamoja na ndege za kivita pamoja na mabomu. Mauzo hayo hutoa maelfu ya nafasi za ajira katika uhandisi nchini uingereza na yameleta mapato ya mabilioni ya pauni kwa biashara ya silaha nchini uingereza. Saudi Arabia imekuwa ikiisaidia serikali ya Yemen inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka mwaka 2015. A�Waasi wa kundi la Houthi ambao ni waaminifu kwa rais aliyenga��atuliwa mamlakani Ali Abdullah Saleh, walianzisha mashambulizi mwaka 2014, na kumfanya rais Abdrabbuh Mansour Hadi kutoroka nchi hiyo kwa muda.