Mahakama yadumisha ushindi wa mbunge wa Emurua Dikirr

Mahakama ya Narok imetupilia mbali kesi iiliyowasilishwa na David keter wa chama cha Jubilee akipinga uchaguzi wa mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ngeno. Katika uamuzi wake jaji Momanyi Bonunga alisema mlalamishi alishindwa kuthibitisha kwamba uchaguzi mkuu wa agosti 8 mwaka uliopita haukuwa wa haki ,huru na kweli .Jaji huyo hivyo basi alimwagiza mlalamishi kulipa shilling million 3 za gharama ya kesi hiyo. Keter alikuwa amemshtaki Ngea��no kwa kuwatisha wapiga kura .Nga��eno alishinda kwa kura 16,098 huku Keter akipata kuraA�A�13,707. Mahakama hiyo hiyo pia ilifutilia mbali uchaguzi wa mwakilishi wa wadi yaA�A�OloposimorumA�A�Wilfred Kuyo. Hakimu mkuu Titus Gesora alisema ameridhika kwamba tume ya uchaguzi a��IEBCA�A�haikuandaa uchaguzi huo wa wadi kwa mujibu wa sheria . Hivyo basi aliagiza uchaguzi huo kurejelewa na IEBC kulipa gharama ya kesi hiyo.