Mahakama iko tayari kushughulikia kesi za uchaguzi-Maraga

Jaji mkuu David Maraga amekariri kuwa idara ya mahakama iko tayari kushughulikia haraka iwezekanavyo, kesi zote zinazohusiana na uchaguzi mkuu wa mwezi agosti. Akiongea na wanahabari baada ya mkutano wa wadau ulioandaliwa na shirikisho la wadau wa sekta ya kibinafsi, Maraga alisema taasisi husika zitachukua hatua madhubuti dhidi ya wale wanaovuruga amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu ili kuepusha visa vya ghasia za uchaguzi hapa nchini.

Akiongea kwenye mkutano huo, kaimu waziri wa usalama wa kitaifa, Fred Matianga��i alisema marehemu David Maraga aliweka mikakati madhubuti ya kushughulikia visa vya uchochezi. Alieleza matumaini yake kuwa uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti utakuwa wa kuaminika, huru na wa haki.

Mkutano huo uliowaleta pamoja waakilishi wa idara ya mahakama, idara ya usalama, tume ya uwiano na mshikamano wa kitaifa na sekta ya binafsi uliandaliwa na shirikisho la sekta ya binafsi kwa ushirikiano na chama cha Mkenya Daima.