Waliopokea Mafunzo Ya Teknoljia Kufuzu

Maafisa waliopokea mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano na uhandisi kwa kipindi cha miezi-12 katika sekta za umma na kibinafsi kupitia mradi wa kidijitali wa afisi ya rais-PDTP, watahitimu leo katika chuo cha mafunzo kwa wafanyikazi wa serikali. Waziri wa teknolojia ya habari na mawasiliano, Joe Mucheru na mwenzake wa elimu, daktari Fred Matianga��i wataongoza sherehe hiyo ambapo wahitimu 100 watapokea vyeti vyao vya kukamilisha mafunzo. Hili ni kundi la pili baada ya la kwanza kuhitimu mwaka uliopita katika mpango uliotekelezwa kwa ushirikiano wa sekta ya umma na ile ya kibinafsi. Kulingana na Mucheru, mradi huo ni muhimu katika kuepusha matatizo ya kiteknolojia katika sekta za umma na kiinafsi. Robert Mugo ambaye ni kaimu afisa mkuu wa halmashauri ya teknolojia ya habari na mawasiliano, amesema kuna mipango ya kuongeza idadi ya maafisa wanaosajiliwa kwa mpango huo, huku maafisa 500 wakitarajiwa kusajiliwa mwaka huu.